Staging

Hatua na wivango

Wakati saratani yako inagunduliwa, madaktari wako wataiweka katika hatua. Hatua hio inaelezea ukubwa wa saratani na jinsi imeenea, na hutumiwa kutabiri mtazamo.


Ductal Carcinoma In-situ (DCIS) kwa wakati mwingine hufafanuliwa kuwa hatua ya 0. Hatua nyingine za saratani ya matiti huelezea saratani vamizi ya matiti (Invasive breast cancer) na ni pamoja na:

Hatua ya 1

Uvimbe hupima chini ya sentimita 2 na tezi za limfu kwenye kwapa haziathariki. Hakuna dalili kwamba saratani imeenea mahali pengine katika mwili.

Hatua ya 2

Uvimbe ufikia sentimita 2 hadi 5, tezi za limfu kwenye kwapa huathirika au zote mbili. Hakuna dalili kwamba saratani imeenea mahali pengine mwilini.

Hatua ya 3

Uvimbe hupima sentimita 2 hadi 5 na unaweza shikamana na miundo kwenye titi kama vile, ngozi au tishu zanazo zunguka, na tezi kwenye kwapa huathirika. Hakuna dalili kwamba saratani imeenea mahali pengine katika mwili.

Hatua ya 4

Uvimbe ni wa ukubwa wowote na saratani imeenea katika sehemu nyingine ya mwili (metastasis).



Huu ni mwongozo uliio rahisishwa. Kila hatua imegawanywa katika kategoria zaidi: A, B na C. Ikiwa huna uhakika unakategoria gani, zungumza na daktari wako.

Mfumo wa upangaji wa TNM


Mfumo wa upangaji wa TNM unaweza pia kutumika kuelezea saratani ya matiti, kwani unaweza kutoa kutoa habari sahihi kuhusu utambuzi.

  • T- Ukubwa wa uvimbe
  • N- Iwapo saratani imesambaa hadi kwenye tezi
  • M- Iwapo satarani imesambaa katika sehemu nyingine ya mwili.


Viwango vya saratani ya matiti


Viwango vinaelezea kuonekana kwa seli zenye saratani.


  • Kiwango cha chini (G1) – seli, ingawa si za kawaida, zinaonekana kukua polepole
  • Kiwango cha kati (G2) - seli zinaonekana kuwa zisizo za kawaida kuliko seli za kiwango cha chini
  • Kiwango cha juu (G3) - seli zinaonekana kuwa zisizo za kawaida zaidi na zina uwezekano mkubwa wa kukua haraka.
Share by: