Saratani ya matiti ni nini?
Saratani ya matiti huanza wakati seli kwenye tishu za matiti au titi huanza kukua nje ya udhibiti. Seli hizi kwa wakati mwingi hutengeneza uvimbe ambao unaweza onekana kwenye kipimo cha mamogramu au kuhisiwa kama uvimbe. Uvimbe huo ni mmbaya kama seli zitakua na kusambaa maeneo yanayo izunguka ama maeneo mengine mwilini. Saratani ya matiti kwa mara mnyingi huathiri wanawake lakini wanaume pia wako katika hatari ya kuathirika.

Dalili za saratani ya matiti
Saratani ya matiti yaweza kuwa na dalili kadhaa. Unapaswa kumuona daktari endapo unakabiliwa na dalili yoyote kati ya hizi:
- Uvimbe kwenye titi au kwapa
- Kubadilika kwa ukubwa au shepu wa titi moja au zote mbili.
- Kutokwa na damu au maji yasiyo ya kawaida kwenye chuchu
- Vibonyo kwenye ngozi ya titi
- Upele kwenye chuchu au karibu na chuchu
- Mbadiliko wa chuchu kama chuchu kuvutwa ndani ya matiti
Kwa wakati mwingi, saratani ya matiti haina uchungu. Hali hii hufanya watu kupuzilia mbali dalili zao zingine za saratani. Kwa hilo, ni vyema kufahamu lililo la kawaida kwako na kumuona daktari wa matiti unapokabiliwa na mabadiliko yoyote.