Uchunguzi

Ugunduzi wa mapema una okoa maisha-Umuhimu wa uchunguzi

Saratani ya matiti katika hatua zake za kwanza ni rahisi kutibu na kuiponya. Ni vyema kufanyiwa uchunguzi kwenye kliniki za matiti hasa unapo kabiliwa na dalili mpya au mabadiliko mapya kwenye matiti. Ku gunduliwa kwa mapema unapunguza haja ya upasuaji wa matiti na chemotherapy kwa sababu ya kuwepo kwa matibabu ya kuhifadhi matiti. Karibia wanawake wote wanao patikana na saratani ya matiti katika hatua za kwanza huishi kwa miaka mitano baada ya kugunduliwa na wana uwezekano wa kuponywa ikilinganishwa na wanawake 3 katika kila 20 wanao gundua katika hatua za mwisho.

Mapendekezo ya uchunguzi kwa wanawake walio na hatari ya wastani* 

*Mwongozo wa Kitaifa wa Uchunguzi wa Kenya, Wizara ya Afya, 2018

Cha kutarajia kwenye kliniki ya matiti

Kwenye kliniki utamwona mshauri wa matiti na muuguzi. Watakuuliza kama umewahi kuwa na shida zozote za matiti na kama una historia ya saratani ya matiti katika familia yako. Mtaalamu ata chunguza matiti yako na chini ya makwapa. Utaelezewa vipimo utakazo hitaji. Vipimo hivi ni kama:


-       Mammogram: hutumia eksirei ya nishati ili kutambua kasoro kwenye titi. Hichi ndicho chombo muhimu Zaidi cha uchunguzi wa matiti kwa kua ina tambua dalili za awali za saratani ya matiti. Mammogram ya mara kwa mara ndio vipimo bora Zaidi vya kugundua saratani ya matiti, mapema wakati mwingine hadi miaka tatu kabla ya kuhisi uvimbe.

-       Ultra-sound: Ultrasound ya matiti hutumia mawimbi ya sauti ya masafa ya juu kutathmini ukubwa na umbo la uvimbe wa matiti na kubaini kama yanaweza kuwa ukuaji wa uvimbe au mifuko ilo jaa majimaji.

Ultrasound ya tezi kwenye kwapa.


-       Biopsy: Ili kupata sampuli ya tishu za matiti. Biopsy inafanywa wakati uchunguzi wa mammograms au uchunguzi wa kimwili unaonyesha mabadiliko ya matiti amboyo yanaweza kuwa saratani. Biopsy ndio njia pekee ya kujua kwa uhakika ikiwa ni saratani. Sampuli za biopsy zitatumwa kwa maabara na daktari maalumu anayeitwa pathologist ataziangalia. Kwa kawaida huchukua siku chache ili kujua matokeo.



copyright 2013 Teresa Winslow LLC
Share by: