Fahamu hali ya kawaida
Ugunduzi wa mapema una okoa maisha
Saratani ya matiti ni mojawapo ya saratani zilizo za kawaida Afrika Mashariki, ambapo lkiwango chake cha vifo ni kati ya zile zilizo za juu zaidi. Inaonekana ikizidi kuathiri wanawake wa umri wa miaka thelathini.
Kwa wastani, saratani ya matiti huanza kuathiri wanawake wa umri mdogo Afrika Kusini mwa Sahara ikilinganishwa na Afrika Magharibi; kwa bahati mbaya, Ingawa ugunduzi na kujulikana kwa mapema upo, nyingi za saratani hizi hugunduliwa kuchelewa kama chaguzi za matibabu ni kidogo, ya bei ghali na sizizo kua na usaidizi.
Ili kuboresha matokea ya saratani ya matiti na kuishi, kugundua mapema ni muhimu
Saratani ya matiti ni nini?
Saratani ya matiti huanza wakati seli kwenye tishu za matiti au titi huanza kukua nje ya udhibiti. Seli hizi kwa wakati mwingi hutengeneza uvimbe ambao unaweza onekana kwenye kipimo cha mamogramu au kuhisiwa kama uvimbe. Uvimbe huo ni mmbaya kama seli zitakua na kusambaa maeneo yanayo izunguka ama maeneo mengine mwilini. Saratani ya matiti kwa mara mnyingi huathiri wanawake lakini wanaume pia wako katika hatari ya kuathirika.
Umuhimu wa uchunguzi
Saratani ya matiti katika hatua zake za kwanza ni rahisi kutibu na kuiponya. Ni vyema kufanyiwa uchunguzi kwenye kliniki za matiti hasa unapo kabiliwa na dalili mpya au mabadiliko mapya kwenye matiti. Ku gunduliwa kwa mapema unapunguza haja ya upasuaji wa matiti na chemotherapy kwa sababu ya kuwepo kwa matibabu ya kuhifadhi matiti.
Hatua na viwango
Wakati saratani yako inagunduliwa, madaktari wako wataiweka katika hatua. Hatua hio inaelezea ukubwa wa saratani na jinsi imeenea, na hutumiwa kutabiri mtazamo. Mfumo wa upangaji wa TNM unaweza pia kutumika kuelezea saratani ya matiti, kwani unaweza kutoa kutoa habari sahihi kuhusu utambuzi.
Tiba za saratani ya matiti
Matibabu kuu ya saratani ya matiti ni ikiwamo na:
• upasuaji
• chemotherapy
• radiotherapy
• tiba ya homoni (pia huitwa tiba ya endocrine)
• dawa za saratani zinazolengwa
• dawa za kuimarisha mifupa (bisphosphonates)
Maumivu ya Matiti
Maumivu ya matiti ni ya kawaida sana kwa wanawake wa umri wote. Kwa yenyewe, maumivu ya matiti hayawezekani kuwa dalili ya saratani.
Wanawake wengi hupata maumivu ya matiti kama sehemu ya mzunguko wao wa kawaida wa hedhi (vipindi). Hii inaitwa maumivu ya matiti ya mzunguko.
Maumivu ya kudumu kwenye matiti ambayo hayahusiani na hedhi yanajulikana kama maumivu ya matiti yasiyo ya mzunguko.
Wakati mwingine maumivu ambayo huhisi kana kwamba yako kwenye titi yanatoka mahali pengine, kama vile msuli wa kifua. Hii inajulikana kama maumivu ya ukuta wa kifua.